Manchester City kukumbana na rungu la FA

0
178

Klabu ya Manchester City imeshitakiwa na chama cha soka cha nchini England FA, kwa kushindwa kuwathibiti wachezaji wake waliomzonga mwamuzi Michael Oliver, katika mchezo dhidi ya Liverpool.

Hivyo Man city, wanaweza kupigwa faini kwa kosa hilo la wachezaji wake tukio hilo lilitokea baada ya mwamuzi kuipa Liverpoool penati.

Oliver alitoa adhabu ya penati baada ya kuona Gary Clichy, amemfanyia faulo Roberto Frimino, katika eneo la hatari na mkwaju huo wa penati ukapigwa na James Milner aliyeukwamisha wavuni.

City wanatakiwa mpaka siku ya Alhamis kuwa wamepeleka utetezi wao kwa chama hicho cha soka cha England.

 Oliver alikupatwa na kadhia ya kuzongwa na wachezaji wa Manchester united wiki iliyopita baada ya kumtoa nje kwa kadi nyekundu kiungo Ander Herrera katika mchezo wa kombe la FA kati ya Man United na Chelsea.

LEAVE A REPLY