Manara awapa pole wakina malinzi baada ya kukamatwa na Takukuru

0
179

Msemaji mkuu wa klabu ya Simba, Haji Manara ametoa salamu za pole kwa viongozi wa TFF ambao wanakabiliwa na kesi ya rushwa.

Manara ametoa pole kupitia akaunti yake ya Instagram kutokana na kukamatwa kwa vinogozi hao ambao ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Mwesigwa Celestine.

Haji Manara amesema sisi kama wanadamu tunapitia changamoto nyingi sana hivyo ni bora tukafarajiana japo hata kwa kupeana pole pale mwenzio anavyopatwa na matatizo.

Ameandika “Poleni Viongozi wangu wa TFF, no matter wat!!ni challenges tu ktk life, bnadaam hatufai kuombeana mabaya,hata kama huwakukutendea haki, Mungu awasimamie kutendewa HAKI,“ameandika Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Haji Manara ambaye alisimamishwa kazi na TFF ya kutokujihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja kwa makosa ya kinidhamu bado anaendelea na msimamo wake wa kuitumikia klabu yake ya Simba kama kawaida kwani alilitaka Shirikisho hilo limpe barua ya kumsimamisha.

LEAVE A REPLY