Manara awajia juu Yanga baada ya kuhoji rufaa ya Mohamed Fakih

0
373

Afisa habari wa Simba, Haji Manara amewataka Yanga kutulia na na kuiacha bodi ya ligi kufanya kazi yake.

Manara amesema kuwa kuna taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga inayoonyesha kuishinikiza Bodi ya ligi kutokutenda haki juu ya rufani yao dhidi ya klabu ya Kagera Sugar.

Kagera Sugar walimchezesha mchezaji Mohammed Fakih aliyecheza dhidi yetu akiwa na kadi tatu za njano ambalo ni kosa kisheria.

Taarifa hiyo ya Yanga iliomnukuu Mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Salum Mkemi aliyeoongea mbele ya waandishi huku akiwa na katibu mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa iliitaka bodi kutokutoa points kwa Simba eti kwa kuwa hizo points zitawaathiri Yanga kwenye kutetea ubingwa wao ambao kwa sasa upo rehani, pia taarifa hiyo imeonyesha Yanga wanao ushahidi kuwa Fakih ana kadi mbili za njano.

Klabu ya Simba inawaambia viongozi wa Yanga wanayo mambo ya msingi ya kuwashughulisha, ikiwepo kutafuta mishahara ya wachezaji wao iliokwama kwa miezi kadhaa kama inavyoripotiwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari,pia waangalie namna bora ya kuurejeshea hadhi uwanja wake wa mazoezi wa Kaunda ili upate kuchezeka tena na sio ulivyo hivi sasa,ambapo umegeuka kama bwawa la kufugia kambale,,ni kushangazwa kulikochupa mpaka kufuatilia rufani isiyowahusu,Hii ni rufani ya Simba dhidi ya Kagera sio wao Yanga.

Tunaamini bodi haitafanya maamuzi kwa shinikizo la yoyote yule,na hatutarajii kuona porojo walizozisema leo zitaondoa ukweli uliopo mezani kwao ambao klabu yetu imeuwasilisha.

Mwisho niwaombe washabiki wetu watulie na waiachie bodi ifanye maamuzi yake ambayo tunaamini yatatoa haki kwa anayestahili.

LEAVE A REPLY