Man Utd yaweka historia mpya ya kupambana na ugaidi michezoni

1
178

Klabu ya Manchester United imeendela kuweka historia kwenye soka la Ulaya na duniani mwaka huu baada ya kuwa timu ya kwanza kuanzisha ajira ya kudumu ya meneja wa kukabiliana na ugaidi.

Nafasi hiyo ya kazi ambayo tayari imeshampata mwajiriwa wake wa kwanza, mkuu wa zamani wa kitengo cha upekuzi cha kituo cha polisi cha eneo Greater Manchester inahusiana na ukabilinaji wa matishio ya ugaidi kwenye viwanja vya michezo hususani nyakati za mechi.

Tangu kuanzishwa kwa nafasi hiyo na kuajiriwa kwa mkurugenzi wake, ukaguzi wa vyombo vya moto na mashabiki wanaoingia kwa miguu umeongezeka kwenye uwanja wa Old Trafford.

Itakumbukwa kuwa mwezi Mei mwaka jana mechi kati ya Manchester United na Bournemouth uliahirishwa na watazamaji kutolewa uwanjani kutokana na tishio la kuwepo kwa bomu uwanjani hapo.

Mwaka jana mtaalamu wa mambo ya ulinzi nchini Uingereza Baroness Ruth Henig alitaka kubadilishwa kwa sheria za utolewaji wa leseni za maeneo ya starehe na burudani ili kuanzisha utaratibu wa mazoezi ya kukabiliana na ugaidi.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY