Man United kupeleka £87m kwaajili ya kumnasa Pogba

0
128

Klabu ya Manchester United inajiandaa kupeleka ofa rasmi ya kumnunua kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba anayechezea timu ya Juventusya Italia.

Baada ya tetesi kuzagaa kwa muda mrefu hatimaye matajiri hao wa Uingereza wanatarajia kupeleka ofa ya kwanza inayokadiriwa kufikia £87m (104m Euros) kwaajili ya kupata huduma za kiungo huyo.

Tayari viongozi wa juu wa klabu ya Juventus wameshakaa kikao pamoja na wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola ili kujadiliana na kukubaliana mambo mbalimbali kuhusu uhamisho huo unaotarajiwa kuwa mkubwa zaidi kwenye medani ya soka.

Taarifa za awali zinathibitisha kuwa kiungo huyo wa zamani wa mashetani hao wekundu ameshakubaliana masuala binafsi na timu hiyo ikiwemo kupata mshahara wa £10.92m (13m Euros) kwa mwaka na uhamisho huo una dalili kubwa za kufanikiwa baada ya miamba ya Hispania, Real Madrid iliyokuwa ikichuana na United kuonyesha nia ya kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha kupata huduma za Pogba.

Wachambuzi wa soka la Uingereza akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Thiery Henry anaamini kuwa uhamisho huo utaiimarisha zaidi ligi ya Uingereza na kuwavutia zaidi wachezaji wengine wenye majina makubwa.

Kocha wa sasa wa Manchester United alimtangaza Pogba kuwa mmoja wa wachezaji wanne vinara anaowawania msimu huu ambapo hadi sasa ameshafanikiwa kuwasajili wachezaji watatu ambaoni Eric Bailly, Henrikh Mkhitaryan na ZlatanIbrahimovic.

LEAVE A REPLY