Man Fongo afunguka ishu ya uchawi kwenye muziki

0
257

Mwanamuziki wa Singeli nchini, Man Fongo amefunguka tetesi za kufanyiwa ushirikina katika muziki wake ili asifanye vizuri na baadhi ya wasanii wenzake.

Man Fongo kuwa hawezi kujua hilo moja kwa moja kwa sababu yeye ndiye msanii mkubwa kuliko wote katika muziki huo ila ushirikina ni kitu ambacho kipo katika muziki.

Amesema kuwa “Katika muziki mambo ya ushirikina yapo lakini huwezi ukamshawishi mtu ukasema mtu fulani hamna ila vitu vinatokea, hivyo ushirikina upo,”.

Ameongeza kuwa licha ya hayo yote hakuna anayeweza kushusha nyota yake kimuziki kwa sasa. Man Fongo kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘La Nafasi’.

LEAVE A REPLY