Mamia wazipinga tuzo za Cesars kwasababu ya Roman Polanski

0
109

Mkanganyiko wa hisia na maoni umeibuka kwa kasi miongoni mwa wapenzi wa filamu nchini Ufaransa kufuatia kuchaguliwa kwa mkongwe Roman Polanski kuwa mkuu wa baraza la majaji wa utoaji wa tuzo za Cesars ambazo ni sawa na tuzo za Oscar.

Director huyo mkongwe ambaye amewahi kushinda tuzo mbalimbali za heshima amekuwa akitakiwa na Marekani kwa zaidi ya miaka 10 baada ya kukiri kufanya mapenzi na mtoto wa chini ya miak 18.

Hata hivyo aliwahi kuondoka Marekani kabla ya hukumu yake mwaka 1978.

Nafasi aliyopewa mwaka huu kwenye tuzo hizo imeyafanya makundi ya haki za wanawake kuita maandamano na kuzigomea tuzo hizo zitakazotolewa mwezi Februari.

Hata hivyo French Academy of Cinema Arts and Techniques ambao ndio waandaaji wa tuzo za Cesars wamempongeza mkongwe huyo.

‘Msanii, mtengenezaji filamu, prodyuza, mwandishi, muigizaji, muongozaji filamu na kuna maneno mengi ya kumuelezea Roman Polanski lakini moja tu la kuelezea kuvutiwa kwetu na further yetu kubwa ni: Ahsante rais. Amenukuliwa akisema hayo mkuu wa French Academy of Cinema Arts and Techniques, Alain Terzian.

Polanski ambaye anafahamika sana kwa filamu zake Chinatown, Rosemary’s Baby na The Pianist ana uraia wan chi mbili, Ufaransa na Poland.

Tuzo hizo za 42 za Cesars zitatolewa jijini Paris mnamo tarehe 24 Februari.

Hadi kufiki Ijumaa tayari watu 50,000 wametia saini pendekezo la mtandaoni la malalamiko juu ya uteuzi huo.

LEAVE A REPLY