Mambo matano usiyoyajua kuhusu mke wa Alikiba

0
4413

Aminah Khalef ni mke halali wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba aliyefunga nae ndoa siku ya jana jijini Mombasa nchini Kenya.

Hapa nakuletea mambo matano muhimu usiyoyajua kuhusu mke huyo wa Alikiba ambaye pia anafahamika kama Aminah Rikesh.

  1. Aminah ana asili ya Uarabuni kwani wazazi wake wana asili ya nchini Oman ambapo ipo kwenye umoja wa nchini za kiarabu.
  1. Licha ya wazazi wake kuwa na asili ya Uarabuni lakini Aminah amezaliwa Mombasa nchini Kenya baada ya wazazi wake kuhamia huko.
  1. Aminah ni mwanamke msomi ambaye amesomea masuala ya biashara na ni mfanyakazi wa kampuni moja jijini Mombasa.
  1. Aminah alikutana na Alikiba mwaka 2016 wakati wa maandalizi ya kampeni za uchaguzi nchini Kenya ambapo Alikiba alikwenda kumpigia kampeni Gavana wa jimbo la Mombasa Hassan Joh ambaye ni rafiki yake wa karibu.
  1. Aminah hakuweka mahusiano yake wazi katika jamii kutokana na mafundisho ya dini yake ya kiislam ambayo inakataza kufanya jambo hilo mpaka ndoa ifanyike.

Alikiba na Aminah Rikesh wamefunga ndoa jijini Mombasa nchini Kenya na sherehe yao kufanyika katika ukumbi wa Dimaond Jubilee jijini Mombasa.

LEAVE A REPLY