‘Mambo ma5’ kuanza kuruka hewani wiki hii

0
271

Kutoka kwa mwanahabari mbunifu na mzoefu mwenye jicho kali la kugundua mahitaji ya hadhira wake kwa wakati muafaka.

Moses Kwindi, ambaye alikuja na kipindi kilichoangazia mabadiliko ya maisha ya binadamu na utamaduni mambo leo na kuanzisha mijadala mipana ya kuijenga vyema jamii ya Tanzania kupitia kipindi chake cha GENERATION sasa anakuja na ‘Mambo ma5’.

Kipindi kipya chenye kuelimisha na kutoa taarifa za mambo muhimu ambayo watazamaji huweka dhana kuwa wanayafahamu kiundani huku ukweli ukiwa ‘hawayafahamu ipasavyo’.

Ni ‘Mambo ma5’ yanayokuonyesha ‘uchache wa ufahamu’ kati ya kile ulichodhani una kifahamu na uhalisia wake.

Kipindi hiki kitakuwa kinarushwa kwenye chaneli ya YouTube ya IshiKistaa kila Ijumaa.

Ongeza ufahamu wa mambo muhimu yanayotokea duniani kupitia ‘Mambo ma5’.

Jiunge na chaneli ya IshiKistaa kupata Mambo ma5 mapya kila wiki.

Elimika na daima uwe wa kwanza kufahamu mambo kiundani!

LEAVE A REPLY