Mama Samia ndani ya ATCL

0
130

Makamu wa rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameonyesha mfano kwa vitendo kwa kuamua kupanda ndege ya shirika la ndege la taifa ATCL kwa safari yake ya kikazi.

Bi. Samia alipanda ndege hiyo pamoja na abiria wa kawaida huku pia akiongozana na msafara wake ambapo aliokoa zaidi ya mil. 30 za bajeti ya ssafari hiyo ambayo ilipaswa kuwa mil. 40 endapo makamu wa rais angeamua kutumia ndege ya kukodi.

Makamu wa rais alikuwa kwenye safari ya kikazi kutoka mkoani Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza huku akinadi kuwa amevutiwa na maoni ya wananchi kuhusu ubora wa huduma zinazotolewa na shirika hilo hivyo akaona ni vyema naye pamoja na msafara wake wazitumie.

Bi. Samia pia alibainisha kuwa sababu nyingine ya kutumia ndege hiyo ni kudhibiti matumizi ya serikali kwa lengo la kuisaidia nchi kufikia kwenye azimio la kuwa na uchumi wa kati.

Makamu wa rais aliambatana na watu 16 kwenye msafara wake na walitumia milioni 7.6 kwa gharama za usafiri huo.

LEAVE A REPLY