Mama Kanumba adai hawezi kuhudhuria harusi ya Lulu

0
611

Mama mzazi wa Steven Kanumba, Florah Mtegoa amesema kuwa hawezi kuhuduria ndao ya Lulu na mmiliki wa EFM Majizo.

Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na tetesi kuwa muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu na mpenzi wake Majizzo wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.

Mama Kanumba amefunguka kuwa, endapo atapelekewa kadi ya mwualiko wa harusi hiyo hawezi kwenda kwa sababu tangu atoke gerezani hawajawahi kuonana na Lulu wala kusalimiana naye.

Mama Kanumba amedai kuwa, hata hiyo habari yenyewe ya Lulu kuolewa na Majizo anaisikia kwenye vyombo vya habari na kwamba hajui lolote.

Mama Kanumba aliweka wazi kutofurahishwa na kitendo cha Lulu kutoka jela mapema baada ya kupata msamaha wa Raisi na kupewa kifungo cha nje mapema mwezi uliopita.

LEAVE A REPLY