Mama Hamisa Mobeto achoshwa na tabia ya Diamond

0
315

Mama mzazi wa Hamisa Mobeto, Shufaa Lutinga amesema kuwa amechoshwa na tabia chafu ya Diamond Platnumz ya kutembea hovyo na wanawake maarufu Bongo.

Kauli ya mama huyo imekuja kufuatia habari za Diamond Platnumz kudaiwa kutoka kimapenzi na warembo, Wema Sepetu na video vixen Bongo, Tunda.

Mama huyo amesema kuwa vitu vyote vinavyoendelea kwenye mitandao ya kijamii havihusiani na mwanaye Hamisa.

Mama Mobeto amesema kuwa kwa sasa kwa upande wao yeye na mwanaye Mobeto hawataki malumbano na kuwekana kwenye mitandao wa kijamii ndiyo maana hawataki kusikia habari zinazomhusu Diamond.

Pia amesema kuwa muda huo  wa malumbano hawana kwa sababu mwanaye anaendelea na maisha yake mengine kabisa ya kutafuta maendeleo na jinsi gani ya kuwalea watoto wake na si kumtegemea mwanaume huyo.

LEAVE A REPLY