Mama Diamond afunguka sababu ya Diamond kutohudhuia msiba wa Godzilla

0
157

Mama mzazi wa msanii Diamond Platinumz amefunguka na kutoa sababu kubwa ya mtoto wake huyo kuacha kwenda katika mazishi ya msanii Godzilla.

Mama mzazi huyo amesema kuwa siyo lazima yeye aende kwa sababu yeye na dada yake walikuwepo kwenye msiba hakukuwa na shida.

Lakini pia mama huyo alisema kuwa sababu kubwa iliyofanya hivyo ni kwa sababu amekuwa akiona misiba mingi ambayo msanii huyo amekuwa akienda , amekuwa akiwateka mashabiki na kujikutwa wakijitoa aktaika msiba na kuanza kumshangaa Diamond platinumz.

Mama Diamond anasema kuwa amekuwa akiona katika misiba , badala ya watu waliokuwa katika misiba hiyo kushiriki katika misiba wamekuwa  wakimshangaa na kumfuata yeye kila sehemu na kuvuruga utaratibu wa misiba.

Mwanamuziki huyo ameshindwa kuhudhuria kwenye msiba wa mwanamuziki mwenzake kutokana na kuwa bize na mambo yake mengine.

LEAVE A REPLY