Mama Diamond afunguka kuhusu kuolewa

0
264

Mama mzazi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond platinumz anaejulikana kama Bi Sandra amethibitisha kufunga ndoa  hivi karibuni.

Mama huyo amesema kuwa kwa muda mrefu walikuwa wakisema amekuwa akionekana na mwanaume akitoka nae na kusemekana kuwa ni mpenzi wake basi ni kweli kuwa mwanaume huyo ni kweli  ndie ataemuoa.

Mama huyo anasema kuwa ni kweli ameolewa na wanaosema kuwa mwanaume huyo ni mdogo kwake wamuache kwa sababu angekuwa mdogo asingeweza kuoa , lakini kwa sababu umri wake unaruhusu ndio maana ameweza kuoa.

Hata hivyo mama huyo anasema kuwa kwa sasa watu wategemee kuona mdogo wake na Diamond anakaribia kuja,kwa sababu watu wanataka mdogo basi na yeye atamuongezea Naseeb mdogo wake wa mwisho.

Pia amesema kuwa ameamua kuweka posti hizo ili kuweza kusisimua watu wanaomfuata waweze kuendelea kumfuata na kuongea mashabiki kwa sababu ustaa ndio unawafanya wao kufanya hivyo.

LEAVE A REPLY