Mama apinga Nandy kuingia kwenye ndoa mapema

0
76

Mama mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Nandy amesema kuwa licha ya Nandy kuwepo katika mahusiano lakini asinpenda kumuona mwanae anaingia katika maisha ya ndoa.

 

Mama Nandy ameweka bayana juu ya maamuzi ya mwanaye kufunga ndoa na msanii mwenzake, Bill Nas ambaye ni mpenzi wake wa muda mrefu sasa.

 

Mama Nandy amesema; “Siwezi kusema tumemkubali Bill Nas au tumemkataa, Nandy ni mtu mzima anachokifanya anakijua, kwa hiyo hatuwezi kumchagulia aolewe na nani, ni uhuru wake kuchagua.

 

“Lakini kwa sasa nisingependelea aingie kwenye mambo ya ndoa kwa sababu ana malengo yake, ana vitu vyake anavyotaka kuvifanya ili afikie mafanikio yake, kwa hiyo mimi naona angefanya kwanza kazi yake, haya mengine yatakuja,” amesema Mama Nandy.

 

Pia mama huyo ameongeza kuwa Nandy ni mtoto ambaye anamsikiliza sana, hivyo kama mzazi anajivunia kuwa na mtoto wa namna ile.

LEAVE A REPLY