Makundi yanayoshiriki Dance 100% yaanza kutambiana

0
83

Baadhi ya makundi yanayoshiriki shindano la Dance100% yameanza kutambiana kila moja likisema ndilo litaibuka na ushindi mwaka huu na kujinyakulia kitita cha milioni 7.

Kundi la The Quest Crew wamesema mazoezi wanayoendelea nayo ni ya nguvu na ufundi wa hali ya juu ambapo wanaamini wataibuka na ushindi.

Mwenyekiti wa kundi hilo Brown Bryton amesema wao wanaamini kwamba ubunifu na kufuata maelekezo ya majaji lazima vitawafanya wanyakue ushindi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kundi la Tatanisha kutoka Mabibo amesema kundi lake limeshabaini udhaifu wa wenzao na ndiyo wanaufanyia kazi na imani yao ni kwamba wao ndiyo watachukua ushindi mwaka huu.

Vile vile Mwenyekiti wa kundi la Ikulu Vegaz, Ramadhani amesema kundi lake ni mara ya tatu kushiriki na nia yao siyo kushiriki kama miaka mingine ila mwaka huu wamepania kuchukua ushindi kwa kuwa makosa waliyorekebishwa na majaji wameyafanyia kazi na wanajiamini kwamba wao ndiyo watatangazwa washindi mwaka huu.

Makundi 10 ambayo yalifuzu hatua ya robo fainali yatashiriki hatua ya nusu fainali wiki ijayo ambapo makundi matano yatabakia katika hatua ya fainali.

LEAVE A REPLY