Makonda awataka wanawake waliotelekezewa watoto kuwa na moyo wa uvumilivu

0
134

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wanawake waliotelekezewa watoto kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki cha mvua.

Paul Makonda ametoa kauli hiyo leo Aprili 13, 2018 alipokuwa akizungumza na umati mkubwa wa mama ambao mpaka sasa hawajafanikiwa kupata namba ya kuingia ndani kusikilizwa shida zao na kuwasii wamama hao kuwa na subira  wapatiwe namba ili zoezi hilo liweze kuendelea kusudi kila mmoja apate haki yake.

Makonda amesema kuwaFuraha niliyonayo nikuona kuna watu wameshaanza kupata amani ya mioyo yao na hilo ndio lilikuwa lengo kubwa la serikali yenu na watumishi hawa waliojitolea ambako kiukweli siwalipi hata senti 5. Lakini zaidi ya yote ndio lengo la Mungu kuleta amani katika familia. Leo ni siku ya Ijumaa ambayo ilikuwa ya mwisho lakini ukitazama kuna watu hata namba hawajapata lakini kuna mambo mawili lazima muyapate”.

Pia amesema kuwa Pamoja na hayo, Makonda ameendelea kwa kusema “jambo la kwanza ni lazima kila mtoto apate kile anachostahili, jingine ni kupata bima ya afya niliyoahidi kwa kila mtoto aliyekanyaga katika viwanja hivi. Kwasababu hizo niwaombe muwe wavumilivu leo wote ambao hamjapewa namba mtapewa. Vumilie mvua najua wakina baba huko walipo wanaombea mvua iendelee kunyesha ili mambo yaharibike lakin waambieni kama mliweze kuvumilia miezi tisa na matusi yote waliyowatukana sembuse mvua ? kwa hiyo tutaendelea kuvumilia mpaka haki itakapopatikana”.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema mpaka kufikia siku ya tano leo wameshasikilizwa takribani wamama 4,000 huku familia 205 kwa hesabu za siku ya jana (Alhamisi) yaani watoto 205 wameondokana na mfumo wa omba omba na sasa wanapatiwa huduma zote zinazostahili kwa baba na mama zao wakiwa pamoja.

LEAVE A REPLY