Makonda awataka wakazi waishio mabondeni Kibulugwa wahame mara moja

0
150

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wananchi wa mabondeni maeneo ya Kiburugwa na Kilungule wahame maeneo hayo kwani ni hatarishi.

Makonda amesema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua uharibifu wa nyumba zilizovunjika maeneo hayo  baada ya wakazi kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.

Pia Makonda amewaagiza Wenyeviti wote wa mitaa kuainisha nyumba zilizojengwa kwenye maeneo hatarishi ambapo amewataka kutoruhisu watu kuendelea kujenga maeneo ya mabondeni.

Katika kutafuta mwarobaini wa tatizo la wananchi waishio mabondeni Makonda ameandaa mkutano wa wananchi wote waishio maeneo ya mabondeni kwaajili ya suluhisho la kudumu.

Katika ziara hiyo amejionea nyumba nyingi zikiwa zimejengwa kwenye maeneo yasiyo rasmi kiasi kwamba hata ikitokea janga la moto inakuwa vigumu Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufika na hata mgonjwa akizidiwa gafla kuwa vigumu kuwahishwa hospital jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.

LEAVE A REPLY