Makonda awapa miezi minne wafanyabiashara wa soko la urafiki kuhama

0
41

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa muda wa miezi 4 kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa Soko Urafiki linalojulikana kama Mahakama ya Ndizi kuhama katika eneo.

Wafanyabiashara hao wanatakiwa kuhama kwa ajili ya kutekeleza agizo la Mahakama kwa kuwa eneo hilo ni mali ya kiwanda cha urafiki.

Makonda amedai kuwa wafanyabiashara hao hawawezi kuhamishwa kama ilivyokuwa awali bali wanatakiwa kuhama baada ya miezi minee kupita.

Pia Makonda amesema wakati huo Serikali itakuwa imeshawaandalia eneo maalum la kwenda ili kuepukana na matatizo kama hayo tena.

Makonda amesema kuwa katika eneo ambalo watapewa litakuwa limeboreshwa zaidi ili wafanyabiashara hao waweze kupata wateja wa kila aina kwa kudai kuwa walipo sasa wanawakosa baadhi ya wateja kutokana na miundombinu ya soko hilo kutokuwa rafiki kwa baadhi ya watu.

LEAVE A REPLY