Makonda atoa onyo kwa watumishi wazembe

0
80

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa mwaka huu wataanza kudili na watumishi wa Umma na wataalam ambao hawafanyi kazi zao vizuri na kuiabisha serikali ya CCM kwa wananchi.

Makonda amesema hayo jana alipokutana na wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam ili kujibu kero na matatizo mbalimbali yanayowakabili ikiwa ni siku ya mwisho kwa zoezi la kupokea na kuzitafutia ufumbuzi kero hizo.

Makonda amedai kuwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni nzuri sana ila watu ambao wanawakwamisha na kuonekana wabaya ni hao wataalam na watumishi ambao wamekuwa wakishindwa kutatua kero za wanachi mbalimbali zinazowafikia maofisini kwao.

Mbali na hilo Makonda alimuakikishia Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wananchi wote waliojitokeza na kutoa malalamiko yao basi watapatiwa majibu yao na kusaidiwa katika matatizo hayo ili kupata haki zao.

LEAVE A REPLY