Makonda aanza maandalizi ya upandaji miti Oktoba mosi

0
180

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefanya ziara katika barabara ya Airport na Barack Obama ikiwa ni maandalizi ya kampeni ya siku ya upandaji miti ijulikanayo kama ‘Mti wangu’ itakayozindiliwa Oktoba mosi mwaka huu.

Makonda amsema miti itakayopandwa Oktoba mosi itamwagiliwa na Mamlaka ya Maji safi na Maji taka nchini (Dawasco) badala ya kutegemea mvua pekee.

Mkuu wa mkoa huyo ameongeza kwa kusema kuwa kila mwananchi anatakiwa kupanda mti na kusimamia ukue ili kufikia lengo la kupanda miti milioni 4.

Pia Makonda aliwahimiza wamiliki wa viwanda kuwa mstari wa mbele katika zoezi hilo la upandaji miti kutokana wao ndio wachafuzi wakubwa wa mazingira hapa nchini.

LEAVE A REPLY