Makamua afiwa na mama yake mzazi

0
17

Msanii wa Bongo Fleva, Makamua amefiwa na mama yake leo hii Juni 29, na msiba upo nyumbani kwao Tabata Kisukulu ambapo anatarajiwa kuzikwa siku ya Ijumaa au Jumamosi.

msanii Makamua amesema chanzo cha kifo mama yake ni matatizo ya Moyo na umauti ulimkuta baada ya kudondoka ghafla.

Pia amesema kuwa “Mama alikuwa na imani sana ya dini, kuna muda alikua akifanyiwa maombi basi anaamini Mungu atamponya na imani yake ilipelekea akaacha kutumia dawa za kutuliza presha jambo lililopelekea moyo wake ukawa unaongezeka ukubwa kila kukicha”

Amesema kuwa “Umauti umemkuta baada ya kudondoka ghafla na alipopelekwa hospitali madaktari waliamuru afanyiwe operationbaada ya vipimo, lakini walipomueka kwenye mashine ya kupumulia ubongo wake ulisoma sifuri kitu kilichoashiria alikua ameshafariki kabla ya kupatiwa huduma”.

LEAVE A REPLY