Majipu matatu yanayoua ‘Bongo Fleva’ na wasanii Bongo

0
712

TEAM VS TEAM

Una timu? Timu ya msanii gani? Kwa fair gani ya mafanikio ya msanii huyo na sanaa kwa ujumla?

Kila msanii wa Bongo Fleva ana timu yake. Timu hizi haziwachangii hela wasanii bali zipo tayari kitumia fedha kibao kuwekeza kwenye bando za intaneti ili ziwatukane wasanii wasiowapenda au wapinzani wa msanii wao. Ziko tayari kukodi usafiri wa gharama na kwenda mbali ili kumshangilia msanii wake na kumrushia makopo msanii wasiyempenda lakini haziko tayari kuchanga hela msanii wao aende studio kuandaa nyimbo.

Akipata tuzo ‘zinakuwa nae’ lakini msanii huyo akiwakosoa mashabiki wake kwa vitendo vya kipuuzi ‘WANAHAMA au WANAMGEUKA’.

RADIO STATIONS ZA WATU NA WASANII WAO

Haiwezekani vitani adui yako akawaambia askari wake kuwa wewe ni mzuri wa mapigano na kuwa hawakuwezi. Na hilo lipo kwenye muziki wa Bongo, karibu kila redio ina aina fulani ya wasanii inaowataka na hususani wasanii wasiofungamana na upande mwingine na hapo ndipo utasikia kila kituo kinamtaka msanii mwenye ‘biff’ na kituo kingine. Kinachofuata? Husikii nyimbo za wasanii fulani kwenye kituo fulani wala interview za wasanii fulani kwenye kituo fulani na hii huenda hadi kwenye mambo ya msingi. Hata msanii ashinde kitu kikubwa kimataifa, baadhi ya vituo ‘HAWATOTAJA HABARI YAKE KAMWE’.

BASATA NA NADHARIA ZA KUKUZA MUZIKI

BASATA kila siku inaona wasanii wakifanya mambo mabaya tu lakini halitoi mkakati wa kuwasaidia wasanii kukua na kupata mafanikio kimataifa.

Kingine wanashiriki kwenye uzinduzi wa tuzo na utoaji wa tuzo na kutoa taarifa za baraza zinazohusiana na pongezi kwa wasanii wanaoshinda tuzo ndani na nje ya nchi.

LAKINI halitoi msukumo chanya kenye masuala ya kurahishisha maendeleo ya sekta ya sanaa. Sio muziki tu, waulize wachonga vinyago, maigizo n.k kama kuna mkakati wa mafanikio ambao wanapewa na BASATA ili wafikie malengo yao.

Majipu haya YATUMBULIWE!!

LEAVE A REPLY