Majambazi wamevamia uwanja wa ndege wa Johannesburg na kuiba mamilioni ya pesa

0
339

Majambazi wenye silaha waliojifanya kuwa polisi wamevamia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Johannesburg nchini Afrika Kusini na kuiba.

Inasemekana majambazi hao waliendesha gari lao mpaka eneo linalozuiwa kuingia na kuchukua makasha ya pesa taslimu.

Makadirio ya pesa zilizoibiwa yanatofautiana, lakini taarifa zinasema kuwa mamilioni ya dola ya sarafu za tofauti tofauti yameibiwa .

Kampuni zinazohudumu katika uwanja wa ndege wa OR Tambo, wenye shughuli nyingi barani, zimethibitisha kwamba wizi huo umefanyika..

Msemaji wa polisi, Athlenda Mathe, amenukuliwa na mtangazaji wa kitu cha Afrika Kusini eNCA akisema kuwa hawezi kutoa kauli ” juu ya kiasi cha pesa kamili zilizoibiwa”.

Walinzi kutoka kampuni ya kibinafsi wanaolinda mali za thamani walizuiliwa na majambazi hao waliokuwa wakisafiri katika gari lenye nembo ya polisi.

Kumekuwa na taarifa kuhusu wizi wa mizigo mingine ya thamani katika miaka ya hivi karibuni kwenye uwanja huo wa ndege

LEAVE A REPLY