Mahakama yamtaka Future kupima DNA

0
137

Mwanamuziki nyota wa Marekani, Future atajuta kupita hovyo, shauri lake na Eliza Reign juu ya kumtelekeza na kutomtunza mtoto ambaye anadaiwa kuzaa na mwanamke huyo limemfika Kooni.

Mahakama mjini Georgia imemtaka Future kupima kipimo cha DNA ili kubaini kama mtoto huyo ni wake au lah. Jaji ametaka vipimo hivyo viwasilishwe kwake mwezi ujao.

Pia kwa amri ya mahakama (Court order) ambayo amepatiwa rapper huyo, ametakiwa kuwasilisha mapato yake na taarifa za kifedha ndani ya siku 10.

Kwa mujibu wa Mwanamke huyo, anadai Future anatengeza hadi Bilioni 43 za Kitanzania kwa mwaka lakini anashindwa kumuhudumia mtoto wake huyo alizaa naye.

Mwanamuziki huyo anatakiwa kupeleka majibu ya DNA hiyo mbele ya mahakama ili kuthibitisha kuwa kama mtoto huyo ni wa kwake au siyo wa kwake.

LEAVE A REPLY