Mahakama yaidhinisha ushindi wa Rais Kenyatta

0
79

Mahakama ya Juu nchini Kenya imeidhinisha ushindi wa Rais Kenyatta na kutupilia mbali kesi mbili zilizofunguliwa kupinga matokeo ya uchaguzi wa awamu ya pili.

Jaji Mkuu David Maraga amesema majaji kwa kauli moja wameamua kwamba kesi zote mbili hazina msingi.

Kesi ya Bw Harun Mwau na wanaharakati wawili Njonjo Mue na Khelef Khalif zimetupiliwa mbali leo na Mahakama kuu jijini Nairobi.

Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa urais wa marudio akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%.

Kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96.

Jumla ya wapiga kura 7,616,217 kati ya jumla ya wapiga kura 19.6 milioni ambao wamejiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo walishiriki uchaguzi huo. Hiyo ni asilimia 38.84.

LEAVE A REPLY