Mahakama yaamuru Wema Sepetu akamatwe

0
788

Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu ametakiwa kukamatwa na mahakama baada ya kukiuka masharti ya dhamana kwenye kesi ya kusambaza picha za ngono.

Maamuzi hayo ya Mahakama yametolewa na Hakimu Maira Kasonde leo baada ya Mtuhumiwa Wema Sepetu kushindwa kufika mahakamani kwa mara nyingine tena, huku kupitia Wakili wake akieleza Wema Sepetu aliugua ghafla akiwa mahakamani hapo.

Akihoji juu ya kutofika mahakamani Hakimu Maira Kasonde ameeleza hata kama amefika Mahakamani, Mahakama isingeweza kujiridhisha kutokana naWema kutotoa taarifa.

Mei 14 2006 Wema Sepetu, pia alishindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kuhudhuria kesi inayomkabili ya kusambaza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii ambapo wakili wake alieleza mshtakiwa huyo ni mgonjwa.

Wema Sepetu anashtakiwa kwa kosa la kusambaza picha za ngono kwenye mitandao ya kijamii. Kesi hiyo sasa imehairishwa tena hadi Julai 4, 2019.

LEAVE A REPLY