Mahakama ya Kisutu waifuta kesi iliyofunguliwa na Hamisa Mobeto dhidi ya Diamond

0
224

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi ya madai ya matunzo ya mtoto iliyofunguliwa na Hamisa Mobeto dhidi ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz baada ya wawili hao kupatana.

Wawili hao leo wamekutana tena mahakamani hapo kwa ajili ya kesi hiyo ya matunzo ya mtoto wa Hamisa aliyezaa na mwanamuziki huyo.

Mahakama imeamua kuifuta kesi hiyo baada ya wawili hao kupata muafaka jinsi ya kulea mtoto wao aliyozaliwa mwaka jana.

Hamisa alifungua kusi hiyo kwa madai kuwa Diamond alikuwa apeleki matunzo ya mtoto kwa mwanamke huyo mpaka kuamua kufunga kesi hiyo.

Hii leo inakuwa siku ya pili kwa Hamisa Mobeto na Diamond kufika mahakamani hapo kwa ajili ya kesi hiyo mpaka leo mahakama kuamua kuifuta kesi hiyo.

LEAVE A REPLY