Mahakama ya Kenya yabatilisha amri ya rais Kenyatta kuhusu wagonjwa wa VVU

0
142

Mahakama ya juu nchini Kenya imepinga agizo la Serikali la kutaka wanafunzi wenye VVU pamoja na wanawake wajawazito wenye VVU watambuliwe na jamii na kudai hiyo ni kinyume cha katiba.

Mahakama imesema kitendo hicho kinavunja haki ya msingi ya ‘usiri’ wa mtu kwa watu wanaoishi na VVU.

Mwaka jana, rais Uhuru Kenyatta aliamrisha majina ya watoto wenye VVU, walezi wao na anwani zao ziorodheshwe ili kuwasaidia kupata huduma bora za afya jambo ambalo hata hivyo wanaharakati walidai litaongeza unyanyapaa.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI, UNAids nchini Kenya kuna zaidi ya watu milioni 1.5 wanaoishi na VVU huku kati yao, 98,000 wakiwa watoto walio chini ya umri wa miaka 14.

LEAVE A REPLY