Mahakama kuu ya Ghana yaitaka Serikali kuweka wazi mkataba wake na Marekani kuhusu wafungwa wa Guantanamo Bay

0
241
Mahakama kuu nchini Ghana imeiamuru serikali ya nchi hiyo kuweka hadharani makubaliano yake na nchi ya Marekani yaliyopelekea kuwakubali wafungwa wawili wa zamani wa gereza la Guantanamo Bay ambao walisafirishwa kurudishwa nchini humo mwezi Januari.
Uamuzi huo wa mahakama kuu umekuja kufuatia mashtaka yaliyofunguliwa na watu wawili walioishtaki serikali kwa kukubali kinyume cha sheria kuwapokea na kuruhusu kuishi nchini humo wafungwa wawili wa gereza la Guantanamo.
Mwanasheria mkuu wa serikali amepinga uamuzi huo na kudai kuwa kufanya hivyo kutapelekea kutahatarisha usalama wa taifa.
Lakini mahakama kuu imekataa hoja ya mwanasheria huyo na kudai kuwa serikali hailindwi na kifungu cha sheria ya usiri ya mwaka 1962.
Wafungwa hao wawili ambao ni raia wa Yemeni, Mahmud Umar Muhammad Bin Atef na Khalid Muhammad Salih Al-Dhuby, walihamishiwa nchini Ghana ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa serikali ya Marekani wa kulifunga gereza hilo.

LEAVE A REPLY