Magufuli: Kenya ndio mshirika nambari 1 wa Tanzania barani Afrika

0
194

Rais John Magufuli amekanusha madai kuwa uongozi wake unajali zaidi matatizo ya ndani na kuwasahau majirani zake.

Rais Magufuli ameyasema hayo kwenye hotuba aliyoitoa mapema leo jijini Nairobi nchini Kenya kwenye ziara yake ya kwanza nchini humo tangu achaguliwe kushika wadhifa wa urais.

Magufuli amesisitiza kuwa amekuwa akiwasiliana na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara kwa mara kwa njia ya simu na bado anaiona nchi ya Kenya kuwa mshirika nambari moja wa Tanzania kwa nchi za Afrika.

Akiwa kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kwenye ikulu ya rais Kenyatta jijini Nairobi, rais Magufuli amesema:

‘Tunazungumza mara nyingi sana kwa njia ya simu lakini kwa kua simu hazionekani na watu ndio maana minong’ono ya aina hiyo inakuwa mingi lakini leo nataka niwaambieni kuwa huwa tunawasiliana sana’.

‘Ziara yangu hapa imekuja kuimarisha uhusiano mwema uliopo tangu zama hizo’.

LEAVE A REPLY