Magic FM yaachiwa huru huku Radio 5 ikifungiwa miezi mitatu

0
180

Kamati ya maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imetangaza hukumu dhidi ya vituo viwili vya Radio vilivyofungiwa kutokana na kile serikali ilichosema kuwa ni kuchochea ghasia na kumkashifu Rais John Magufuli.

Vituo vilivyokuwa vimefungiwa kwa muda usiojulikana kwa tuhuma za kukiuka Sheria za Utangazaji ni Magic FM cha jijini Dar es Salaam na Redio 5 cha jijini Arusha.

Kupitia maamuzi yaliyosomwa na Makamu mwenyekiti wa kamati ya maudhui, Joseph Mapunda Kamati imeikuta Redio 5 na hatia ya kumkashifu rais na kuchochea uvunjifu wa amani na hivyo imehukumiwa kulipa shilingi milioni 5.

Radio 5 imefungiwa kutorusha matangazo kwa miezi mitatu na kuwekwa chini ya uangalizi wa mwaka mmoja.

Wakati huo huo Radio Magic FM imepewa onyo na kutakiwa kumwomba radhi rais wa Tanzania pamoja na wasikilizaji wa redio hiyo kwa siku tatu mfululizo.

Tarehe 29 Agosti mwaka huu Waziri wa Habari nchini, Nape Nnauye alitangaza kuvifungia vituo hivyo viwili vya redio kwa muda usiojulikana kwa madai kuwa vilikiuka sheria za utangazaji.

LEAVE A REPLY