Madeleine Albright kuingia kwenye Uislam endapo Trump atatekeleza sera ya kuwabagua Waislam

0
187
DCSW108

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani, Madeleine Albright na staa wa filamu ya Big Bang Theory Mayim Bialik wamesema kuwa wao watajiunga na Uislam endapo rais wa Marekani, Donald Trump atatetengeneza orodha ya waislam raia wa nchi hiyo.

Albright na Mayim Bialik wamekaririwa wakisema ‘kaa tayari, jiandae’ kujiandikisha.

‘Nilizaliwa mkatoliki, nikawa Episcopalian na baadae nikaja kugundua kuwa familia yangu ni wayahudi’ ameandika Bi. Albright ambaye ni mwanamke wa kwanza kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

‘Nimejiandaa kujiandikisha kuwa Muislam kwenye #mshikamano’ baada ya kuandika hivyo tweet hiyo ikapata makumi kwa maelfu ya ‘likes’.

Maneno hayo ya Bi. Albright yamekuja kufuatia tetesi zinazoendelea kuzagaa kuwa rais Trump anatarajia kusaini hati ya amri ya rais itakayopelekea kuwepo kwa upekuzi wa kupita kiasi, kuzuia wakimbizi na kuzuia watu kutoka nchi saba duniani kutoingia nchini humo.

Ingawa watu wengi wamejitokeza na kuanzisha kampeni ya mtandaoni ya #to stand in solidarity with America’s Muslim population baada ya Trump kushinda uchaguzi wa Marekani lakini maneno ya Abright yanatajwa kuwamasisha wengi kuelezea hisia na misimamo yao juu ya hatua hiyo inayotarajiwa kufanywa na rais huyo.

LEAVE A REPLY