Madee afunguka sababu ya Dogo Janja kufunga ndoa ya siri

0
190

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Madee amefunguka sababu iliyowafanya wafanye siri kufungwa kwa ndoa ya Dogo Janja na muigizaji Irene Uwoya.

Madee amesema walijua kuwa wawili hao ni maarufu, hivyo taarifa za ndoa yao ingewashangaza wengi na kuharibu mipango yote.

“Nilijua ni habari kubwa, ni habari ambayo ingeleta purukushani kwa wanahabari hata ndoa yenyewe isingefanyika, na hata wale ambao tumewaalika tulijua hawa wana marafiki zao ambao ni wana habari, hivyo tulichokifanya ni kutengeneza usiri wa ile shughuli, hata tuliowaalika tuliwaambia mnakuja hapa lakini simu zenu wekeni hapa, unangia unashuhudia tukio lakini hauna ushahidi wa kupeleka kwa wengine”, .

Madee ameendelea kwa kusema kwamba iwapo wasingefanya siri huenda wangetokea watu wa kuwashauri vinginevyo, na ndoa hiyo isingefungwa.

“Tungesema tuanze kuwaalika wangeanza kuwashauri usikubali kuolewa na yule au kumuoa huyu, ile ndoa ingekufa na sisi tungepata dhambi”.

Mwezi Novemba mwaka 2017 msanii Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa, jambo ambalo  liliwashtua watu wengi, huku wengine wakisema ni kiki ya filamu.

LEAVE A REPLY