Madee afunguka mwanawe kufanya muziki

0
129

Mwanamuziki Bongo Fleva, Madee amesema iwapo mwanawe wa kike aitwae Aimal Hamad atachagua kuwa msanii litakuwa ni jambo la kawaida na hawezi kumzuia.

Madee amesema kuwa atamruhusu kufanya muziki kwasababu hata yeye amefuata nyayo za baba yake katika fani hiyo.

Mwanamuziki huyo amendelea kusema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi kwenye Sanaa kwa wanawake lakini hana budi kumruhusu kuonyesha kipaji chake kwa kuwa kila mtu amepangiwa ridhiki yake.

Pia Madee amewashauri wazazi wenzake kuwaangalia watoto wao wafanye kitu wanachotaka kwa upande wake hawezi kumpangia mwanae kazi ya kufanya kwani ana maamuziki yake.

Madee amesema kuwa hawezi kumpangia mtoto wangu kitu cha kufanya katika maisha yake, akitaka muziki sawa kwani hayo ni maisha yake.

LEAVE A REPLY