Madee afunguka kuhusu ndoa yake

0
135

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Madee amefunguka na kusema kuwa hawezi kufunga ndoa kwa kufuata mkumbo kisa Fulani kaoa na yeye ndiyo aoe.

Madee amesema kuwa ataoa pale atakapojaliwa kuoa lakini si kuangalia Fulani kaoa na yeye ndiyo aoe hivyo hawezi kufanya.

Mwanamuziki kutoka pande za Manzese amesema kuwa hawezi kufunga ndoa kwa kufuata mkumbo kisa staa fulani amefunga ila atakachofanya ni kufanya sapraiz siku yoyote kuanzia sasa na kufunga bila kutangaza.

Madee anayebamba na Ngoma ya Sema amesema kwa sasa hafikirii kuoa kwani bado anaangalia lebo yake ya Manzese Music Baby (MMB) hiyo iweze kutanuka zaidi na tayari amefanikiwa kwa msanii Gaza na Dogo Janja ambao ‘wameshasimama’.

Pia Madee amesema kuwa ndoa si jambo la kukurupuka hivyo unatakiwa ujipange kabla ya kuamua kufunga ndoa ili usije ukajutia uamuzi wako.

LEAVE A REPLY