Mabasi ya Mwendokasi yasitisha huduma za usafiri

0
100

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, (UDART) imesitisha huduma zake kwa baadhi ya njia kuanzia saa 11:00 alfajiri.

Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi.

Aidha, kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Kimara – Morroco, Kimara – Magomeni Mapipa, na Gerezani – Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa.

Hata hivyo, Kampuni hiyo kupitia kwa mkuu wa kitengo cha mawasiliano, Deus Bugaywa imeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

LEAVE A REPLY