Maandamano ya kumpinga rais Kabila yafanyika Kinshasa

0
392

Waandamanaji wameweka vizuizi na kuchoma magari katika mji mkuu wa Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya maafisa wa polisi kuwazuia kuandamana.

Waandamanaji hao wanamtaka rais Joseph Kabila ajiuzulu baada ya kukamilika kwa muhula wake mnamo mwezi Disemba 20 mwaka huu.

Upinzani unahofia kwamba bwana Kabila ana mpango wa kuchelewesha uchaguzi wa urais unaotarajiwa mwezi Novemba ili kusalia madarakani.

Maafisa wa uchaguzi na serikali wanasema kuwa uchaguzi huo utaahirishwa kutokana na matatizo ya mipango katika taifa hilo la Afrika ya kati.

Taifa la DRC halijawahi kuwa na ukabidhi wa mamlaka ulio huru tangu uhuru wake zaidi ya miaka 45 iliopita.

LEAVE A REPLY