Lyyn akubali kufanya kolabo na Tanasha

0
46

Video vixen ambaye amegeukia muziki wa Bongo Fleva, Irene Godfrey maarufu kama Lyyn amefunguka na kusema kuwa yupo tayari kufanya ngoma na Tanasha Donna kwani hana tatizo naye.

Lyyn amesema kuwa haoni tatizo kufanya kolabo na Tanasha hata kama naye aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond Platnumz kipindi cha nyuma.

“Sina tatizo na Tanasha ikitokea tutafanya tu kolabo, yeye ni msanii na mimi pia ni msanii kwa hiyo tunaweza kufanya tu hiyo haina shida,” alisema Lyyn.

Pia Lyyn amesema kuwa aliachana na Diamond kitambo kabla hata hajaanza kufanya muziki na haoni tatizo kushirikiana na mrembo huyo ambaye anammiliki Mondi kwa sasa.

Lyyn ambaye alianza kupata umaarufu baada ya kutokea kwenye video ya wimbo wa kwanza wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny kutoka WCB na baada ya wimbo huo kila mtu akaanza kumfahamu mrembo huyo.

LEAVE A REPLY