Lulu na Mobetto wamaliza bifu lao

0
102

Muigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael na Mwanamitindo Hamisa Mobetto wameonyesha kuwa hawana bifu na kila mtu hana kinyongo na mwenzake.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi Februari 23, 2019 katika utoaji wa tuzo za  Filamu Zetu International Festival Film (SZIFF) mwaka 2019  ambapo Lulu alimuita kwa mbwembwe jukwaani Hamisa Mobeto.

Lulu ambaye alikuwa Mshehereshaji (MC) kwenye Shughuli hiyo aliyofanya katika ukumbini wa Mlimani City, alimuita kwa mbwembwe na kusababisha kuibuka kwa shangwe kwa watu waliokuwa ukumbini hapo.

Lulu alianza kwa kumtambulisha Hamisa kwa kusema ‘Ninamleta kwenu mrembo, model, mama wa Watoto wawili jukwaani na si mwingine bali ni Hamisa Mobetto’.

Baada ya kupanda stejini Hamisa alienda kukabidhi tuzo kwa moja ya washindi na kurejea kukaaa katika siri yake.

Hamisa na Lulu walishawahi kuingia kwenye bifu zito baada ya Hamisa kumtuhumu Lulu kwa kumuibia aliyekuwa Mpenzi wake Majizzo lakini Hamisa alitangaza kuwa hana kinyongo na Lulu.

LEAVE A REPLY