Lulu hakuwa na ndoto ya kuishi na mwanaume mwenye mtoto

0
76

Muigizaji wa Bongo Movie, Elizaberth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa haikuwa ndoto yake kuanza maisha na mwanaume ambaye tayari anamtoto na mwanamke mwengine.

Lulu amefunguka hayo wakati akimpa ushauri shabiki yake ambaye amerudiana na mpenzi wake wa zamani na kumkuta tayari anamtoto

Lulu ameandika kuwa “Mimi kwenye maisha yangu sikuwahi kutamani kuanza familia na mtu mwenye mtoto tayari.

Lakini nikaja kugundua kuwa binadamu hatujakamilika. Wakati mwengine sio mpaka uwe kilema ndio uonekane haujakamili kuna mambo mengine yanaweza kusimama kama kilema. Hili la kuwa na mtoto kabla ya ndoa linaweza kusimama kama kilema”.

Lulu akaendelea kwa kuandika lazima ujiulize maswali haya kabla ya kuamua kuwa na mtu mwenye mtoto/watoto tayari. La kwanza “Unampeda.

Ni mtu anaweza kuwa na wewe kwa kila hali?, Anakusaidia kukusogeza mbele kiakili na kimaisha?, Anakupa furaha na ana support ndoto zako.

LEAVE A REPLY