Lulu Diva: Nisingehangaika na muziki ningekuwa najiuza

0
238

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa muziki umemsaidia kutoingia katika biashara ya uchangudoa.

Lulu Diva ameushukuru muziki na kusema kuwa  kama asingefanya juhudi binafsi katika muziki wake angekuwa miongoni mwa wanawake wenye mwonekana hasi kwa jamii.

Lulu Diva amesema kuwa awali alikuwa na ndoto za kuamini uzuri wake umetosha kumfanya aishi mjini, kitu ambacho kilikuwa mawazo potofu, kwani anaamini kama angeendelea hivyo asingeweza kufikia ndoto zake.

Hivi sasa Lulu Diva anafanya vizuri katika tasnia ya Bongo fleva na pia amepata mafanikio makubwa ikiwemo kununua Nyumba na gari zuri.

LEAVE A REPLY