Lulu Diva kuachia albam

0
76

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa anatarajia kuachia albam yake ya kwanza baada ya kuingia kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Hayo yanajiri baada ya kufanya vizuri kwa EP yake ya The 4Some ambayo imepokelewa vizuri na mashabiki wake wa muziki huo.

Diva amesema kuwa, kutokana na mabadiliko makubwa katika soko la kazi za wasanii kupitia online, hii imemfanya mapema mwaka 2021 kufikiria kuachia album yake ya kwanza.

Lulu Diva amezitaja ngoma zake GuguGaga na Come Again kuwa ndio ngoma zilizoweka rekodi nzuri zaidi ya mauzo kwenye EP yake hiyo.

LEAVE A REPLY