Lulu Diva, Belle 9 na Bonge la Nyau wapata ajali

0
67

Wasanii wa Bongo Fleva, Lulu Diva, Belle 9 na Bonge la Nyau wamepata ajali ya gari alfajiri ya leo maeneo ya Ubena Chalinze mkoani Pwani wakati wakiwa njiani kurejea jijini Dar es Salaam wakitokea Iringa.

Lulu amethibisha na kusema; “Ni kweli tumepeta ajali, tulikua tunaendeshwa, mimi nimeumia kichwani nimevimba ila Belle 9 ameumia zaidi, amewaishwa hospitali kwa matibabu.

Bonge la Nyau ameumia kiasi. Kwa sasa nipo Polisi kuchukua PF3 kisha nimfate Belle 9, Hospitali.

Bonge la Nyau alisema kuwa “Sijui chanzo ni nini maana wakati ajali inatokea nilikua nimelala nikaja kushtukia gari imeacha barabara na kupinduka, Belle 9 anaonekana ameumia mgongo na kichwani,”.

Naye Bonge la Nyau kupitia ukurasa wake amesema; “Mwenyezi mungu ametunusuru kwenye Ajali mbaya ilotokea mida hii tukiwa njian maeneo ya ubena chalinze.

LEAVE A REPLY