Lulu Diva aonyesha ndinga yake ya kifahari

0
44

Mwnamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amedhihirisha kama yeye ni The Boss Baby baada ya kuonekena akitembelea gari lake la kifahari aina ya Jeep.

Lulu Diva amesema gari hiyo ameinunua na ina thamani ya Milioni 300 za kitanzania pia rangi yake haifanani na gari la msanii yeyote hapa Bongo.

Aidh Lulu Diva ameendelea kusema kama kuna mtu yeyote anayebishia gari lake kama amenunua kwa bei hiyo anaweza aka-google kuangalia gharama za bei hizo ili kupata uhakika.

Kwa ndinga hii inadhihirisha kuwa kwa sasa Lulu Diva ndiyo anaongoza kumiliki gari yenye thamani kuliko msanii yeyote wa kike hapa Tanzania.

Hapo awali gari hiyo ilikuwa inafananishwa na gari ya mwanamuziki mwenzake wa Bongo Nandy lakini msanii huyo amesema kuwa gari hizo hazifanani kabisa.

LEAVE A REPLY