Lulu Diva akanusha kuwa na bifu na Nandy

0
72

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amesema ugomvi unaodaiwa ulikuwepo kati yake na msanii mwenzake Faustina Mfinanga ‘Nandy’ ni wa kitoto tu.

Lulu Diva amesema siku zote panapokuwepo wanawake zaidi ya wawili, hakukosekani maneno ya hapa na pale, hivyo ndiyo maana kukatokea ‘kaugomvi’ ambako hata hakakuwa na msingi wowote.

“Sidhani kama nilikuwa na ugomvi wa maana kati yangu na Nandy, yaani ni ugomvi tu wa ki-mwanamke, hauna maana yoyote na pia hakuna kitu kibaya kama maneno ya kuambiwa, hivyo niko vizuri tu na Nandy na haipendezi kioo cha jamii kugombana hovyo,”

Kwa siku za karibuni, wawili hao walikuwa kwenye sintofahamu huku chanzo kikiwa hakifahamiki kwa undani.

LEAVE A REPLY