Lulu Diva aiomba Serikali kuwafikilia wasanii kuhusu Tamasha la Fiesta

0
357

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva ameiomba Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam iwafikilie wasanii ambao wataondolewa katika Fiesta baada ya muda wa Tamsha hilo kufika mwisho saa sita.

Wiki iliyopita mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku kupigwa mziki sehemu za wazi ambapo amesema kuwa mwisho unatakiwa kuwa saa za usiku na siyo kukesha.

Lulu Diva ni mmoja wa wasanii ambao walokuwa wakinufaika na tamsha hilo kwa sababu kwanza ndio mara yake ya kwanza  kufanya show katika tamsha ilo amabpo alipata bahati  ya kutumbuiza katika baadhi ya mikoa iliyopita.

Mwanamuziki huyo amethibitisha kuwa kutokana na mabadiliko hayo ya ratiba yeye pia ni mmoja wa wasanii waliokatwa kutumbuiza katika show hiyo kubwa ambayo kwake ingekuwa ni ndoto kwa kuifanya kwa mara ya kwanza kwenye mkoa mkubwa wa jijini Dar Es Salam.

Lulu Diva anmeomba serikali kuwafikilia kwa sababu  kulipwa kwake kunategema watu wengine wengi nyuma yake na ukizingatia kuwa kwake ilikuwa ni kama ndoto kufanya show katika jukwaa kubwa kama hilo.

Kwa uapnde Ruge Mutahaba alisema kuwa kwa ratiba hiyo ni lazima wapunguze idadi ya wasanii  watakao perfom siku iyo ili kuweza ku-balance muda unaotakiwa. Lakini bado alitoa tumaini kuwa kuna uwezekana wa kupata kibali cha kupitisha mud na ikitokea kibali kikapatikana basi wataweza  kuweka wasanii wote waliopangwa.

Tamasha la fiesta linategemea kufanyika tarehe 25 Novemba katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam na baadhi ya wasanii ambao mpaka sasa wapo katika orodha ni pamoja na Alikiba, Vannesa mdee, Madee, Fid Q, Weusi, Nandy, Ben Pol.

LEAVE A REPLY