Lulu Diva afungukia urembo wake

0
144

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amesema kuwa anapenda urembo na mwili wake ni sehemu moja wapo ya biashara zake katika harakati zake za kutafuta pesa na maisha.

Lulu Diva amesema mwili wake ni biashara kwa sababu watu wengi wanamshabikia na watu wengi wanampenda kutokana na kujirusharusha kwenye video.

Amesema kuwa “Mwili wangu biashara kwa sababu naweza nikaitwa mahali kwa sababu ya muonekano wangu wanavyoniona na wakanilipa pesa.

Pia amesema kuwa wengine wanapenda jinsi nilivyo na ninavyojirusharusha kwenye video halafu msanii anatakiwa awe na muonekano kuanzia mavazi hadi maisha yake nje ya muziki” Lulu Diva

Aidha msanii huyo ameongeza kusema yeye  anapenda sana urembo na kama mtu hatampenda kwenye muziki basi atampenda kupitia muonekano wake ambao unapatikana katika mwili wake.

 

LEAVE A REPLY