Lulu Diva afungukia kutelekeza mtoto

0
164

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka juu ya tuhuma za kutelekeza mtoto akisema kwamba taarifa hizo hazina ukweli kwani hajawahi kuwa na mtoto.

Lulu Diva amesema kwamba suala la kuwa na mtoto halina siri, na iwapo kuna mtu anamjua mtoto aliyetelekezwa basi ampeleke ili aishi naye.

Pia Lulu Diva amesema kwamba hawezi kumlaumu TID kwani anazeeka, huku akimtaka kuacha kuzungumza mambo ambayo hayana uhakika kwa kuwa sio vitu alivyozoeleka kuvifanya.

“TID siwezi kumlaumu anaanza kuzeeka, amekaa muda mrefu sana kwenye game, kitu kama mtoto ni vitu ambavyo automaticaly lazima kitaonekana, Lulu ana mtoto nimtupe nimpeleke wapi.

Lulu Diva ameendelea kusema, “T.I.D asinitafute ubaya, ameanza lini kuimba taarabu kwa sababu sio muziki wake, hi ni taarab unafanya kwa sababu unaongea kitua ambacho si kweli”.

LEAVE A REPLY