Lulu Diva afunguka kuumizwa na skendo ya kutoka na Mavoko

0
353

Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ‘Amezoea’ Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa aliumizwa na taarifa za kutoka kimapenzi na Rich Mavoko.

Kauli hiyo ya Lulu Diva imekuja baada ya siku chache kusambaa taarifa na picha za mwanamuziki huyo zikidai kutoka kimapenzi na mkali kutoka WCB, Rich Mavoko.

Lulu Diva amesema kuwa yeye kama binadamu ishu hiyo ilimuumiza sana kwa kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu hilo kwani Rich Mavoko ni rafiki yake.

Rich Mavoko
Rich Mavoko

Mwanamuziki huyo amesema kuwa siku aliyoonekana katika mapozi ya kimahaba ilikuwa ni usiku wa show ya Fiesta jijini Dar es Salaam ambapo kwake kujiachia ni jambo la kawaida na si kama alikuwa kwenye mahusiano na mwanamuziki huyo.

 Lulu Diva amesema kuwa baada ya kusambaa picha hizo aliumia sana lakini amejikaza kwa kuwa ishu imeshatokea japokuwa Mavoko ni rafiki yake.

LEAVE A REPLY